Jamii ikijifunza pamoja

BIDII ACADEMY · BIDII YANGU

Mwongozo wa Bidii

Kila kitu kinaanza na mimi. Ninatenga muda wa kujifunza, ninatumia maarifa na ninawajibika kwa hatua zangu — hiyo ndiyo Bidii yangu.

Safari ya mwanafunzi

  1. 1

    Jisajili na thibitisha barua pepe

    Fungua Jisajili, jaza taarifa na manenosiri yanayofanana, kisha kubali sera ya faragha. Thibitisha barua pepe kupitia kiungo unachopokea. Akaunti ya mwanafunzi haihitaji idhini ya msimamizi.

    Endelea
  2. 2

    Kamilisha wasifu na tathmini

    Weka taarifa zako za wasifu na eneo. Jibu tathmini kwa ukweli na eleza malengo yako ili mapendekezo ya masomo yawe na manufaa. Tathmini hii si alama ya mikopo.

    Endelea
  3. 3

    Chagua kozi na soma kwa mpangilio

    Fungua Masomo, chagua kozi na moduli. Maandishi ndiyo mwanzo; video, sauti na kazi zinapatikana pale zilipoandaliwa. Sababu ya somo kufungwa huonyeshwa katika safari yako.

    Endelea
  4. 4

    Fanya jaribio na wasilisha kazi

    Jaribio linahitaji 70% au zaidi. Somo lenye kazi linahitaji kazi kuwasilishwa; si kusubiri ukaguzi. Somo linalofuata hufunguka baada ya masharti ya somo kutimizwa.

    Endelea
  5. 5

    Tumia maarifa katika Daftari

    Bidii yangu ni kurekodi matumizi yote kila siku na kutenganisha fedha binafsi na biashara. Ninaandaa bajeti yangu ya siku, wiki na mwezi na kuishi ndani yake. Katika Daftari, mauzo ya mkopo ni deni la kupokea, mkopo si mapato na makosa husahihishwa bila kufuta historia.

    Endelea
  6. 6

    Fuatilia maendeleo yako

    Angalia masomo na majaribio uliyokamilisha. Vyeti hutegemea kutimiza masharti ya kozi, pamoja na kuwasilisha kazi zilizowekwa. Cheti si dhamana ya mkopo, ajira au ithibati ya kitaaluma.

    Endelea

Kila jukumu lina nafasi yake

Kiongozi wa KEEN

Fungua KEEN na tengeneza kikundi. Weka jina na eneo, kisha nakili kiungo cha mwaliko au tuma kwa WhatsApp. Waombaji wanaingia kwa kiungo au kodi; wewe huidhinisha wanachama na kuweka matangazo.

Vikundi vya KEEN

Mkufunzi

Katika Maudhui, andaa kozi, moduli, masomo, maswali na kazi. Ukaguzi unaonyesha kazi zilizowasilishwa: soma, toa maoni, kisha weka Imefaulu au Inahitaji Marekebisho. Vikundi vinahitaji upangiwe na msimamizi.

Maudhui

Msimamizi

Ingia kwa akaunti yenye jukumu husika. Usimamizi wa vikundi, maudhui, fedha, masoko na wabia hutegemea ruhusa. Super Admin pekee hubadili majukumu ya wafanyakazi na bei; siri za huduma haziwekwi ndani ya kurasa.

Ingia kama msimamizi

Pesa Bila Daftari Hupotea Bila Habari

Anza kwa miamala yako halisi ya leo. Usichanganye pesa za nyumbani na biashara. Historia yako ni binafsi; mkufunzi, mshirika na wabia hawaoni Daftari lako kwa sababu tu wana jukumu kwenye jukwaa.

Maswali yanayoulizwa mara nyingi

Kila kitu kinaanza na mimi.

Bidii yangu — najifunza, natekeleza, nawajibika.

Jisajili